Uchunguzi wa Panorama: Masuala mapya yaibuka juu ya uhusiano wake Mo Farah na Alberto Salazar



Maswali mapya yameibuka juu ya uhusiano baina ya Mo Farah na kocha wake wa zamani Alberto Salazar yaliyojitokeza katika uchunguzi mpya wa kipindi cha BBC Panorama.
Nyaraka zinaonyesha kuwa farah alikanusha mara kwa mara kuwa alidungwa sindano za madawa ya kututumua misuli michezoni ya L-carnitine kabla ya mbio za London Marathon 2014, alipoulizwa na wachunguzi wa shirika la Marekani la kupambana na madawa hayo (Usada).
Farah baadae alibadili maelezo yake kwa wahunguzi wa Usada, akisema kuwa alikua amesahau.
Nyaraka pia zilifichua jinsi maafisa wa riadha wa Uingereza walivyopelekwa nchini Uswisi kukusanya madawa yanayokubalika kisheria kutoka kwa mtu aliyefahamiana na Salazar.
Baruapepe ambazo Panorama ilizipata zinaonyesha ni jinsi gani maafisa wa riadha wa Uingereza walivyoelezea awali hofu yao juu ya ikiwa sindano hiyo ilikua salama ''kimichezo''
Kipindi cha Panorama ' Sakata ya Mo Farah na Salazar' itaangaliwa Jumatatu , 24 Februari.
Salazar anaendesha mradi wa Nike Oregon - ambako kumekuwa nyumbani kwa mshindi wa marambili wa Olypmpiki Farah kuanzia 2011 hadi 2017.
Mwaka 2015 uchunguzi wa Panorama kwaushirikiano na wavuti wa Mrekani ProPublica, mara ya kwanza ulifichua madai ya matumizi ya madawa ya kusisimua misuli michezoni ya Salazar, kocha ambaye alisifiwa kwa kiasi kikubwa kwa kumsaidia Farah kuwa mwanariadha bora zaidi Muingereza.
Bingwa wa medali za dhahabu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio Mo Farah
Image captionBingwa wa medali za dhahabu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 katika mashindano ya Olimpiki mjini Rio Mo Farah
Kipindi kiliibua uchunguzi wa Usada , uliosababisha Salazar kuwekea marufuku ya miaka minne ya kutoshiriki micheo na mahakama ya mizozo ya kimochezo nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka 2019.
Salazar anakana matokeo ya uchunguzi na amekata rufaa dhidi ya marufuku iliyowekwa dhidi yake.
Katika taarifa yake alisema kuwa : "Jopo lilisema kwamba nilifanya kwa 'nia njema' na bila 'nia mbaya ya kukiuka sheria na maadili '.
Sheria mbili zilizokiukwa na Salazar zinahusiana na matumizi ya njia zilizopigwa marufuku ya za kuchomwa dawa ya L-carnitine, ambayo ni dwa inayokubalika kisheria.
L-carnitine ni kichocheo halisi halisi kisicho na madhara ambacho hubadilika na kuwa amino acid, ambayo, mtu akichomwa inakwenda moja kwa moja katika mishipa ya damu, baadhi ya watafiti wanasema kinaweza kuharakisha kuongeza nguvu za mwili na kuinua ubora wa mwnariadha kimchezo.
Matumizi ya kichocheo hicho yaliruhusiwa miongoni mwa sheria za Shirika la kupambana matumizi ya madawa ya kututumua misuli michezoni duniani (Wada) ambapo kiwango kilichokubalika ni chini ya mililita 50 kila baada ya saa sita.
Mwaka 2014, Farah alimaliza mbio akiwa wa nane katika mbio zake za kwanza za london Marathon.
Miaka mitatu baadae, wakati gazeti la Sunday Times liliporipoti kwamba alipokea kichocheo cha L-carnitine, the Digital, Culture, Media, na ukafanyika uchunguzi wa Kamati maalumu ya Michezo ya 'kupambana na matumizi ya madawa ya kututumua misuli michezoni' iliita timu ya Farah mbele yake kutoa maelezo.
Kamati ilihakikishiwa kuwa kiasi cha mililita 13.5, zilikua ni kikomo cha kiwango kinachokubalika, kwa mujibu wa dokta Charaverty, licha ya kwamba alishindwa kurekodi vipimo. Hakuna ushahidi kuwa sheria yoyote ilivunjwa.
Mo FarahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFarah alimaliza mbio akiwa wanane katika mbio za London Marathon mwaka 2014

Ushahidi mpya

Ushahidi wa Panorama unatoa mwangaza zaidi juu ya hali na unaibua maswali kuhusu ushawishi wa Salazar.
Baruapepe kati ya maafisa wa kumbambana na dawa za kuongeza nguvu katika siku za mwanza kabla ya mbio za marathon walifichua hofu zao juu ya uchomaji wa sindano hiyo kwa mwanariadha.
Tarehe 6 Aprili 2014, Fudge liliandika: "Huku mchakato huu unakubalika kabisa na manunu za Wada kuna madai ya kifilosofia juu ya ikiwa hii ni 'sawa katika 'moyo wa michezo…'."
Aliongeza: "Ingawa Alberto na Mo wana matarajio kuhusu kufanya hili, hatujafikia kiwango ambapo... hatuwezi kujiondoa."
Mkurugenzi wa zamani wa utendaji katika shirika la kupambana na madawa ya kututumua misuli michezoni Neil Black anakiri "kuwa haifurahishi kwa kiasi fulani".
Aliandika "…kwani ni lazima tuwe tunapitia mchakato wa dawa hizi tukiwa tumekaribia kabisa mashindano ya London Marathon ? ... Hiyo ni baada ya hata tufikirie kuhusu moyo wa michezo."
Dkt Chakraverty alionekana kuwa mwenye hofu juu ya uwezekano wa "athari."
Aliandika "… ingekua vizuri kama tungeijaribu kwa mtu fulani kwanza."
" Naelewa [Salazar] yuko makini lakini … tunapaswa kuwa tunamuuliza kufuata ushauri huu."
Uamuzi ulitolewa wa kuendelea kuitumia. Lakini kulikua na tatizo: dawa yenye kichocheo L-carnitine waliyoitaka haiwezi kupatikana nchini Uingereza. Hapo ndipo Salazar anapohusika.
Salazar alianzisha mawasiliano baina ya Fudge na mtu aliyefahamiana nae Switzerland ambaye aliweza kuagiza dawa iliyofanyiwa vipimo ya L-carnitine katika muundo uliohitajika.
Mo Farah aandikisha historia kwa kushinda dhahabu ya mbio za mita 10,000, Rio 2016Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMo Farah alishinda dhahabu ya mbio za mita 10,000, Rio 2016
Walikana.
Wakati wanariadha wanapofanyiwa uchunguzi, wanapaswa kuorodhesha matibabu yote na dawa ambazo wamezitumia katika kipindi cha siku saba zilizopita. Farah alifanyiwa vipimo siku sita baada ya kudungwa sindano -tarehe 17 Aprili 2014. Licha ya kuorodhesha idadi ya bidhaa na mdawa, alishindwa kureko kuwa alitumia kichocheo cha L-carnitine katika fomu ya udhibiti wa matumizi ya madawa ya kututumua misuli.
Mwaka mmoja baadae, kama sehemu ya uchunguzi dhidi ya Salazar, wapelelezi wa Marekani (Usada) walifika London kufanya mahojiano na maafisa wa shirika la Uingereza la kukabiliana na madawa ya kuongeza nguvu michezoni UKA - na Farah.
Maafisa wa Usada walikaa na Farah kwa takriban saa tano- na kipindi cha Panorama ilipata karatasi ya mahojiano hayo.
Aliulizwa swali mara nyingi ikiwa alikua amechomwa sindani ya L-carnitine katika London Marathon, Farah alikana.
Aliulizwa: "Kama mtu alisema kwamba ulikua unatumia sindano ya L-carnitine, anasema uongo ?"
Farah alisema: "Kabisa atakua hasemi ukweli , 100%. Sijawahi kutumia sindano ya L-carnitine kabisa ."
Halafu aliulizwa: "Una uhakika kwamba Alberto Salazar hajakwambia uchome sindano za dawa ya L-carnitine?"
Farah alijibu: "Hapana, sijatumia kabisa sindano za L-carnitine."
Dakika kadhaa baada ya mahojiano hayo, Farah alikutana na Fudge, ambaye alikua amehojiwa na Usada siku moja kabla.
Halafu Farah akarudi haraka kwenye chumba cha mahojiano wakati wachunguzi walipokua wakijindaa kutoka. Akabadilisha maelezo yake.
Farah aliiambia Usada: "Nilitaka tu kueleweka wazi, samahani, niliitumia wakati ule na nilidhani sikuitumia...''
Akaulizwa: "Kwahivyo ulipokea L-carnitine… kabla ya London marathon?"
Farah akajibu : "Yaa."
Aliongeza kuwa : "kulikua na mazungumzo mengi kabla … na Alberto wakati wote alikua akifikiria juu ya ' Kile ambacho ni kizuri zaidi ?' 'Kile ambacho ni bora kwangu?'"
Mwaka 2015, Wanariadha wa Uingereza walifanya tathmini juu ya madai ya Panorama. Licha ya mwenyekiti wa taasisi ya udhibiti wa matumizi ya madawa ya kutitimua misuli ya Uingereza UKA Ed Warner kuiambia BBC wiki hii kwamba alishauriwa Farah atengane na Salazar,tathmini ilibaini kuwa "hakuna sababu ya hofu " juu ya Salazar kuendela kwa kocha wa Farah.
Uchunguzi mpya wa Uingereza UKA reunaendelea kubaini ikiwa kuna makosa yoyote yaliyofanyika katika kushughulikia suala la tuhuma dhidi ya Farah.

BM

BM