Ikiwa bado kuna mechi 13 zimesalia, huku Barcelona ikiongoza dhidi ya Real Madrid kwa alama mbili, Mechi ya El Clasico huko Bernabeu siku ya jumapili inaweza kuwa muhimu katika kuwania taji la La Liga inayolitafuta kwa miaka sasa.
Hakuna timu ambayo imeonekana kuwa na ushawishi zaidi msimu huu, timu zote mbili zimekuwa katika wakati mgumu, na Real kwa sasa wana mashindano ya ligi ya mabingwa huku wakiwa wamepoteza katika uwanja wao wa nyumbani, kuna mengi ambayo yanaweza kutokea katika mchezo huu ambao unaonekana kuwa mgumu na ushindi unawaniwa sana.
Haya ndio mambo yanayoangaziwa kwa kina kuelekea mtanange huo wa Jumapili.
Je, Benzema anaweza kuonyesha maajabu na kuwainua Real?
Kitu ambacho kimeonekana kigumu kwa Real msimu huu ni ugumu wa kupata magoli, ambapo wikendi iliopita ilidhihirika walipoifunga Levante goli 1-0 huku wakishindwa kufumania nyavu mara nane msimu huu. Katika hatua za mwanzo za kuwania kikombe hicho, Karim Benzema aliweza kuibebea timu yake kwa kiwango kikubwa.
Mchezaji huyo wa Ufaransa alifunga magoli 13 katika michezo ya kwanza 16, mengi akiyafunga ndani ya eneo la hatari.
Lakini Benzema amefunga goli moja tu katika ligi tangu wakati wa krismasi la muhimu zaidi, ni ushindi wa mwisho wa mechi dhidi ya Atletico Madrid na hakuna mchezaji aliyeweza kushika nafasi yake.
| Wachezaji waliofungia Real katika michuano ya La Liga ukiondoa magoli ya penalti |
|---|
| 11 - Benzema |
| 3 - Casemiro, Kroos, Modric |
| 2 - Bale, Ramos, Rodrygo, Varane, Vazquez, Jovic, Valverde |
| 1 - Vinicius, Carvajal, Nacho, Isco, Hazard, Rodriguez |
Takwimu zinaonyesha kuwa katika msimu huu, ukiondoa magoli yaliyopatikana kwa njia ya penati hakuna mchezaji wa Real aliyeweza kufunga zaidi ya magoli matatu katika ligi.
Sergio Ramos ni mfungaji kinara wa pili akiwa na magoli matano lakini magoli matatu kati ya hayo alifunga kwa mikwaju ya penalti.
Washambuliaji wa timu hiyo wameonekana kutofanya vizuri msimu huu kwa upande wa kupata magoli: Gareth Bale (alipata magoli mawili katika ligi), Eden Hazard (1), Luka Jovic (2), Rodrygo (2) na Vinicius Junior (1) wote hawakufanya vizuri katika kipindi hiki, na kuwafanya viungo kama Toni Kroos na Fede Valverde pamoja na mlinzi Ramos kusogea mbele na kusaidia kupatikana kwa magoli.
Kufikia sasa, ukosekanaji wa magoli mengi unasingiziwa kusababishwa na uwepo wa majeruhi wengi na mwishoni mwa wiki iliyopita walipocheza na Levante, walirudi nyuma tena baada ya kiungo mshambuliaji Eden Hazard kuumia ambapo alikua amerejea kutoka kwenye majeraha.
Hali hii ni tofauti na wakati Real inasimamiwa na Zidane miaka kadhaa iliyopita, timu ilikuwa haifanyi vizuri lakini ilikuwa haikosi magoli.
Shukrani nyingi kwa Cristiano Ronaldo ambaye kwa wakati mwingine aliibeba timu mabegani mwake kwa kuamua mchezo.
Barca inasumbuliwa na majeruhi na chaguo la kikosi
GETTY IMAGES
Barcelona itawakosa wachezaji wake wa chaguo la kwanza walinzi Sergi Roberto na Jordi Alba kwa sababu za majeruhi.
Nafasi zao zitachukuliwa na walinzi ambao hawafanyi vizuri sana Nelson Semedo na Junior Firpo ingawa kulikuwa na hofu ya Gerard Pique baada ya kuumia siku ya Jumanne walipobanwa mbavu na Napoli kwa goli 1-1.
Meneja wa sasa Quique Setien ameweka wachezaji wengi wa kumsaidia nyota wao Lionel Messi, ambaye ameweza kuibeba timu yake katika msimu huu na kupata jumla ya magoli 18 na kuchangia mengine 12.
Katika mchezo dhidi ya Napoli katikati ya wiki, Setien aliamua kumchezesha Messi na Antoine Griezmann katika eneo la ushambuliaji.
Huku katika eneo la kiungo akiwa amewajaza Sergio Busquets, Ivan Rakitic, Frenkie de Jong na Arturo Vidal.
Anaweza kuchagua kikosi hicho hicho wikiendi hii lakini ni kama tu nafasi ya kufanya hivyo itakuwepo.
