TYSON AMLAMBISHA SKAFU BINGWA WA DUNIA KWENYE NDONDI.

Tyson alionyesha umahiri wake katika ulingo wa ndondi baada ya kumaliza ufalme wa Deontay Wilder wa miaka mitano akithibiti taji la ukanda wa WBC katika uzani mzito duniani baada ya kumwangusha binngwa huyo kwa njia ya knockout katika raundi ya saba.
Katika mechi iliochezewa katika Mecca ya ndondi mjini Las Vegas nchini Marekani raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 31 alimshinda mpinzani wake katika pigano ambalo ni wachache wangeweza kutabiri..
Mchanganyiko wa ngumi za kulia na kushoto ambazo Wilder amekuwa akizitumia kuwalambisha sakafu wapinzani wake zilitumika dhidi yake na kuangushwa katika raundi ya tatu na tano.
Fury alihakikisha ametimiza aliyoahidi na kubadili mbinu zake kutoka upigaji hadi mwenendo wake na kumzidia nguvu mpinzani wake ambaye hajawahi kushindwa.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Tyson ameandika: "Nataka kusema Deontay Wilder, ameonyesha weledi wake. Amepigana hado raundi ya saba. Yeye ni shujaa, atareja tena kuwa bingwa. "Lakini mfalme amerejea katika kiti chake."
Je huu huu utakuwa ni wakati wa mwisho Deontay Wilder kuwa kwenye mpambano? Amekuwa bingwa wa dunia tangu january 2015.
Je atajaribu tena kurejesha taji lake? ama pengine mambo kwenda mrama katika raundi ya saba kutahitimisha taaluma ya raia huyu wa Marekani?
Tyson Fury ametimiza kile alichosema atafanya na kile ambacho wengi walikuwa na mashaka ikiwa anaweza kutimiza.
Alitawala pambano hilo na kuonyesha kwanini alihitaji sana kuongeza uzito na pia sababu ya yeye kubadilisha makocha kila mara.

BM

BM