Arsenal huenda ikalazimika kumuuza mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang ikiwa watashindwa kufikia makubaliano kuhusu masharti ya mkataba mpya, mchezaji huyo mkataba wake utakwisha mwaka 2021. (Star)
Kocha wa zamani wa Everton Sam Allardyce amesema alijaribu kumsajili Aubameyang kutoka Borussia Dortmund kabla ya mshambuliaji huyo kujiunga na washika bunduki (Talksport)
Winga wa England Jadon Sancho, 19, anaweza kusalia na Dortmund baada ya msimu huu ingawa alikuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Chelsea, Liverpool au Manchester United. (Ruhr Nachrichten - in German)
Leicester City inafikiri kumpatia mkataba mpya Christian Fuchs, 33, wakati mchezaji huyo wa nafasi ya ulinzi akikaribia kumaliza mkataba wake.
